Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wameongeza dozi katika ligi kuu ya NBC wakiichapa Pamba Jiji mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa AAzam Complex
Beki Ibrahim Bacca ameendeleza kuweka hai malengo yake ya kuwania tuzo ya ufungaji bora msimu huu leo akifunga bao lake la pili likiwa ni bao la uongozi kwa Yanga katika dakika ya 5
Unaweza kusema ilikuwa mechi ya upande mmoja kwa muda mwingi Pamba Jiji wakipaki basi
Kazi nzuri ya Jean Baleke aliyeanza leo iliinufaisha Yanga kwa kupata mkwaju wa penati mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada kuvutwa ndani ya eneo la hatari
Stephane Aziz Ki alifunga penati hiyo na kuiandikia Yanga bao la pili
Kipindi cha pili Yanga iliendelea kulisakama lango la Pamba na kufanikiwa kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa Maxi Nzengeli na Kennedy Musonda
Nzengeli amefunga bao lake la tatu leo akiwa kinara wa kuzifumania nyavu kwa upande wa wachezaji wa Yanga
Ni Alama 12 kwa Yanga ikiendelea kusalia nafasi ya nne, Djigui Diarra akiandikisha 'cleansheet' ya nne msimu huu