Droo ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa imefanyika leo ambapo Yanga imeangulia kundi A pamoja na timu za TP Mazembe, Al Hilal na USM Alger
Hili ni kundi ambalo kama kocha Miguel Gamondi atachanga karata zake vyema, Yanga ina nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
TP Mazembe na Al Hilal ndio timu zinazoonekana kuwa tishio zaidi huku MC Alger wakiwa hawatabiriki
Misimu miwili nyuma Al Hilal waliiondosha Yanga katika hatua za awali ligi ya mabingwa na kuangukia kombe la Shirikisho ambako Wananchi walipangwa na TP Mazembe hatua ya makundi
Wakati huu Yanga inakwenda kuchuana na Al Hilal katika hatua ya makundi lakini ikiwa na kikosi imara zaidi kuliko vile ilivyokuwa mara ya mwisho timu hizo zilipokutana
Msimu uliopita TP Mazembe walicheza nusu fainali ya michuano hii lakini sio timu ambayo Yanga inaweza kuihofia kwa sababu hata Wananchi nao msimu uliopita wangeweza kufika nusu fainali kama sio zile fitna walizofanyiwa katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns
Sio kundi jepesi lakini pia sio kundi la kuwafanya Wananchi wahofie kwani nafasi ya kwenda robo fainali ipo