Baada ya ligi kuu ya NBC kusimama kupisha kalenda ya FIFA, wachezaji 12 wa Yanga wamejiunga na timu za Taifa kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2025
Mechi hizo zitaanza kupigwa Alhamisi Oktoba 10 na kuhitimishwa Oktoba 15
Mshambuliaji Prince Dube akiwa na kikosi cha Zimbabwe watakuwa ugenini Oktoba 10 kuchuana na Namibia Oktoba 10
Oktoba 10 pia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itakuwa ugenini DR Congo kuchuana na wenyeji wao katika mchezo wa tatu kundi H
Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mudathir Yahya na Clement Mzize ni sehemu ya wachezaji katika kikosi cha Stars
Stephane Aziz Ki akiwa na Burkina Faso, Oktoba 10 wako nyumbani kuikaribisha Burundi
Kennedy Musonda na Clatous Chama wao wako katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia ambayo itashuka dimbani Oktoba 11 nyumbani kuchuana na Chad
Oktoba 11 pia Duke Abuya akiwa na timu ya Taifa ya Kenya watakuwa ugenini dhidi ya Cameroon wakati Khalid Aucho akiingoza Uganda kumenyana na Sudan Kusini nyumbani. Djigui Diarra nae atakuwa nyumbani na Mali akiikabili Guinea Bissau
Aziz Ki atamaliza majukumu yake ya timu ya Taifa Oktoba 13 katika mchezo dhidi ya Burundi utakaopigwa Ivory Coast
Duke Abuya, Prince Dube na Djigui Diarra watamaliza majukumu yao Oktoba 14 wakati wengine waliobaki watamaliza majukumu yao Oktoba 15
Habari njema ni kuwa nyota watano walio na Stars mechi marudiano dhidi ya DR Congo itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa hivyo hawakuwa na changamoto ya kusafiriΒ
Ikumbukwe mchezo unaofuata baada ya kalenda ya FIFA ni Kariakoo dabi dhidi ya Simba Oktoba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa