Baada ya kukamilisha majukumu ya timu za Taifa, sasa kituo kinachofuata ni Simba
Jumamosi Oktoba 19, nyasi za uwanja wa Benjamin Mkapa zitawaka moto kwa mchezo wa Kariakoo Derby, Yanga ikisaka ushindi wa nne mfululizo dhidi ya watani zao Simba
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kunyakua alama zote tatu ili kusogea juu katika msimamo wa ligi malengo yakiwa pale kileleni
Wachezaji 12 wa Yanga waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa wanatarajiwa kuingia kambini leo kuungana na wenzao kwa ajili ya maandaizi ya mwisho
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hii sio mechi ya kuamua mbio za ubingwa kwani bado mapema lakini alama tatu anaamini zitakiweka kikosi chake katika nafasi nzuri kwenye mbio hizo dhidi ya Simba
Kama Yanga itashinda mchezo wa Jumamosi na kushinda mchezo wake wa kiporo itakuwa mbele ya Simba kwa tofauti ya alama tano
Tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa tangu juzi ambapo VIP A ni Tsh 50,000/- (zimeisha), VIP B Tsh 30,000/-, VIP C ni Tsh 20,000/-, Orange Tsh 10,000/- na Mzunguuko Tsh 5,000/-
Mchezo utapigwa saa 11 jioni....!