Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema kikosi kinaendelea kujifua Avic Town ambapo leo watakamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kulikuwa na hofu kuhusu beki Ibrahim Bacca aliyepata majeraha madogo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2025 dhidi ya DR Congo akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania
Walter amesema Bacca na wachezaji wengine waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa wamerejea wakiwa salama, mchezaji pekee ambaye ni majeruhi ni Farid Mussa ambaye pia alianza mazoezi mepesi juzi
"Hakuna taarifa yoyote ya majeruhi kwa wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa. Wote wamerejea wakiwa salama"
"Mtu pekee ambaye bado ni majeruhi kikosini ni Farid Mussa ambaye pia ameshaanza mazoezi mepesi"
"Zaidi ya hapo hakuna taarifa nyingine ya majeruhi kutoka katika kikosi chetu. Tuko imara tayari kwa dabi siku ya Jumamosi," alisema Walter