Kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli leo ameibuka nyota wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Nzengeli ndiye aliyesababisha bao pekee la ushindi kwa Yanga baada ya shuti lake kumgonga mlinzi wa Simba Kelvin Kijiri na kujaa kimiani
Hiyo ni tuzo ya pili ya mchezaji bora wa mechi Nzengeli anabeba msimu huu
Pongezi zaidi wanastahili wachezaji wote wa Yanga kuanzia mlinda lango Djigui Diarra, safu yake ya ulinzi na wachezaji wengine waliohakikisha ushindi unapatikana leo
ADVERTISE HERE