Bao la Jean Baleke limetosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Ulikuwa mchezo mgumu kama ilivyotarajiwa, nafasi zilitengenezwa chache lakini Yanga imeonyesha sifa ya mabingwa, kushinda hata mechi ambazo haichezi vizuri
Alama tatu muhimu ambazo zinaerejesha Yanga katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 21
Aidha ni cleansheet ya kwanza kwa mlinda lango Aboubakar Khomein aliyekaa langoni leo badala ya Djigui Diarra
Yanga imecheza mechi saba, imeshinda zote pasipo kuruhusu bao
ADVERTISE HERE