Wakala wa wachezaji Yao Kouassi na Pacome Zouzoua ametua nchini kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo ya mikataba mipya ya nyota hao, imefahamika
Zambro Traore ambaye pia ni Wakala wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, atakuwepo Zanzibar leo kushuhudia mchezo wa ligi kuu kati ya Singida Black Stars dhidi ya Yanga utakaopigwa saa 2:30 usiku katika uwanja wa New Amaan Complex
Mikataba ya Pacome na Yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini Yanga imedhamiria kuwaongeza mikataba mapema
Kumekuwa na tetesi za hapa na pale kuhusu wachezaji hao lakini jambo la uhakika ni kuwa tayari Rais wa Yanga Injinia Hersi Said yuko mbiono kuhuisha mikataba yao