Yanga imeendeleza ubabe katika ligi kuu ya NBC baada ya leo kuichapa Singida Black Stars bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex
Shuti la Pacome Zouzoua nje kidogo ya 18 katika dakika ya 67 lililosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu katika mchezo uliotawaliwa na ubabe mwingi kutoka kwa wachezaji wa Singida BS
Yanga iliwapoteza walinzi wake wa kushoto Chadrack Boka na Nickson Kibabage ambao waliumizwa
Alama tatu muhimu ambazo zinaepeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza msimu huu
Ushindi wa nane mfululizo kwa Yanga bila ya kuruhusu bao..!