Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza msimu huu dhidi ya Azam Fc, kikosi cha Yanga kinarejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Tabora United
Alhamisi Novemba 07 Yanga itashuka dimba la Azam Complex kumenyana na Tabora United katika mchezo utakaopigwa saa 12 jioni
Yanga bado iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 24 baada ya kushuka dimbani mara 9
Ni wazi vijana wa kocha Miguel Gamondi watahitaji kushinda mchezo dhidi ya Tabora United ili kuhakikisha wanakwenda kwenye majukumu ya timu za Taifa wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi
Aidha mwishoni mwa mwezi huu mechi za hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa zitaanza kupigwa Yanga iikifungua dimba kwa kuikabili Al Hilal ya Sudan katika mchezo utakaopigwa Novemba 25/26