Baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc, uliopigwa Novemba 02, mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wanatarajiwa kucheza mechi nyingine nne katika mwezi huu wa Novemba 2024
Keshokutwa Alhamisi, Naovemba 07 Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex kumenyana na Tabora United ambapo baada ya mchezo huo ligi itasimama kwa takribani wiki mbili kupisha kalenda ya michuano ya CAF kufuzu Afcon 2025
Wananchi watarejea tena uwanja Novemba 21 kuikabili Fountain Gate katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Azam Complex
Novemba 25/26 Yanga itaanza kampeni ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal mchezo wa kwanza ukipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga itahitimisha Novemba kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa Novemba 29 huko Ruangwa