Baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, beki Ibrahim Bacca atakosekana katika kikosi cha Yanga kwenye mechi tatu za ligi zinazofuata
Mchezo wa kwanza ni kesho dhidi ya Tabora United utakaopigwa uwanja wa Azam Complex
Bacca atakosa mechi nyingine mbili baada ya mapumziko ya kalenda ya CAF ambapo Yanga itahitimisha mwezi huu kwa mechi dhidi ya Fountain Gate na Namungo Fc
Hata hivyo Bacca atakuwepo dimbani kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika mechi mbili za kuhitimisha kampeni ya kuwania tiketi ya kufuzu Afcon 2025 dhidi ya Ethiopia na Guinea
Mechi dhidi ya Azam Fc ilipelekea kadi nyekundu na kadi nyingi za njano kwa wachezaji wa Yanga ambao waliadhibiwa na mwamuzi Ahmed Arajiga kila walipolalamikia maamuzi yake
Walinzi wote wa kati Bakari Mwamnyeto, Dickson Job walionyeshwa kadi za njano. Pia yumo mlinda lango Djigui Diarra, kiungo Khalid Aucho na mshambuliaji Prince Dube
Stephane Aziz Ki alipewa kadi ya njano akiwa yuko benchi baada ya kutolewa nje akiadhibiwa baada ya kupinga maamuzi ya Arajiga