Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jioni ya leo itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kumenyana na Guinea katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2025
Ni mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi Tanzania ikihitaji ushindi ili kukata tiketi ya kufuzu kwa michuano hiyo kwa mara ya tatu katika historia
Tanzania iko nafasi ya tatu kundi H ikiwa na alama 7 huku Guinea wakiwa nafasi ya pili wakiwa na alama 9
Guinea wanahitaji alama moja tu kufuzu hali inayofanya mchezo huo kuwa mgumu
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 10 jioni na hautakuwa na kiingilio baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk. Samia Suluhu Hassan kutoa ofa kwa mashabiki kushuhudia mchezo huo bure
Kila la kheri Stars..
ADVERTISE HERE