Mdhamini/Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohammed 'GSM' leo ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ambapo amesafiri hadi Kibaigwa mkoani Dodoma kufanya maadhimisho ya siku huu
GSM ameadhimisha siku hii akiwa na watoto wa shule ya Msingi Mzogole, Kibaigwa ambapo alitoa misaada mbalimbali ili kuboresha mazingira ya shule hiyo
Akizungumza kwa niaba yake, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisema upendo kwa jamii ndio umemsukuma GSM kusafiri zaidi ya kilomita 400 hadi Kibwaiga kwa ajili ya maadhimisho ya siku hiyo
"Kwa kipekee leo ni siku ya kuzaliwa ya Mdhamini na Mfadhili wetu Ghalib Said Mohamed( GSM) na kwa upendo mkubwa aliokuwa nao akaamua kutoka takriban kilometa 400 kuja hapa Kibaigwa kufurahia na watoto wa shule ya Msingi Mzogole"
"Kwa nafasi aliyo nayo angeweza kwenda nchi yoyote. Huenda inaweza kuwa sehemu ya ndoto ya watoto wengi wa hapa ambao pengine baadae wanaweza kuwa wafanyabiashara wakubwa kama yeye"
"Pamoja na kwamba amekuja kwa lengo la kufurahia nanyi siku ya leo, Rais wa GSM ametoa kiasi cha Tsh 40m kwa ajili ya maboresho ya madarasa mawili pamoja na madawati 300, matundu mawili ya vyoo, viti na meza 12. GSM pia ametoa kiti cha kutembelea kwa binti anayeishi na ulemavu. Klabu ya Yanga pia itatoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya michezo," alisema Hersi








