Al Hilal watua mapema Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Nov 2024
Al Hilal watua mapema Dar

Wapinzani wa Yanga katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika, Al Hilal wamewasili nchini leo kuelekea mechi ya kwanza ya makundi CAF CL

Yanga itakuwa mwenyeji wa Al Hilal katika mchezo wa kwanza kundi A ambao utapigwa Jumanne ijayo, Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua Dar, Kocha Mkuu wa Al Hilal, Florent Ibenge, amesema wamekuja mapema Dar ili kuzoea hali ya hewa na pia kupata muda wa maandalizi ya mchezo huo

Ibenge amebainisha kuwa kikosi chake kiliwakosa nyota wengi ambao walikuwa katika majukumu ya timu za Taifa, hivyo watatumia siku zilizobaki kufanya mazoezi ya pamoja kabla ya mchezo dhidi ya Yanga

Wakati Al Hilal wakitua, Yanga imejichimbia Avic Town ikijiandaa na mechi hiyo chini ya Kocha Mkuu Sead Ramovic ambaye alianza kazi ya kuinoa Yanga juzi Jumatatu akichukua nafasi ya Miguel Gamondi aliyefutwa kazi

Nyota ambao walikuwa katika majukumu ya timu za Taifa wanatarajiwa kuanza kuripoti kambini Avic Town leo kuungana na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo muhimu kwa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
30m ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’