Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra ameweka rekodi ya kibabe katika mechi za kufuzu Afcon 2025 zilizomalizika mapema wiki hii Mali ikiwa miongoni mwa timu 24 zilizofuzu kwa fainali za michuano hiyo zitakazofanyika mwakani huko Morocco
Diarra alikaa langoni katika mechi zote 6 za Mali akifanikiwa kuondoka na 'cleansheet' tano akiruhusu bao moja tu
Ni yeye na mlinda lango wa Senegal Edouard Mendy walioruhusu bao 1 tu katika michuano hiyo
Diarra ameungana na nyota wengine wa Yanga ambao wamezisaidia timu zao kufuzu kwa michuano hiyo
Dickson Job, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya, Clement Mzize, Khalid Aucho, Clatous Chama, Kennedy Musonda, Stephane Aziz na Prince Dube wameshiriki kikamilifu katika kuhakikisha mataifa yao yanafuzu kwa Afcon 2025
Nyota hao wanatarajiwa kuungana na wachezaji wengine wa Yanga Avic Town kuendelea na maandalizi ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan
Mchezo huo utapigwa Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa...