Hii ni mechi yetu sote - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2024
Hii ni mechi yetu sote - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Yanga, Ali Kamwe, amesema wanafahamu mechi dhidi ya Al Hilal itakuwa ngumu hivyo amewataka wanachama na mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaongezea hamasa wachezaji wao

Akiendelea kuwahamasisha mashabiki wa Yanga katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi dimba la Mkapa siku ya Jumanne, Kamwe ameeleza umuhimu wa mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaongezea ari wachezaji

Β "Ni mechi ngumu, lakini kwa ukubwa wetu na umoja wetu, wanachama na mashabiki wakiungana, wakijazana uwanjani kwa kuwashangilia wachezaji wetu, tutaifanya kuwa nyapesi, wachezaji na benchi la ufundi wapo tayari kwa vita hii," alisema Kamwe

Aliongeza wachezaji wao watarajiwa kupambana na kuhakikisha wanampokea kocha mpya kwa ushindi na si matokeo mengine

"Wale waliokuwa katika vikosi vya timu ya taifa tunajua wengi walicheza kwa hiyo bado wana utimamu wa mwili, kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Al Hilal, kwa maana hiyo haitampa shida sana kocha wetu, kinachotakiwa hapo ni muunganiko tu ili kupate ushindi kwenye mchezo wa kwanza ambao ni muhimu sana," alisema Kamwe

Aliongeza hawana hofu na mchezo huo licha ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Tanzania Bara na badala yake wataongeza umakini kuelekea mchezo huo

"Hatuna hofu na mechi hii eti kwa sababu tulipoteza mechi zilizopita, badala yake imetufanya sasa tuwe makini kwenye michezo yote inayofuata, hatutadharau mechi wala hatutaingia uwanjani kwa mazoea," Kamwe alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’