Mamia ya mashabiki wa Yanga wamesafiri hadi mkoani Lindi kushuhudia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa leo katika uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa
Hii ni kama mechi ya fainali kwa Yanga, baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo, hakuna nafasi kwa Yanga kupoteza alama zaidi
Wanasema afe kipa, afe beki, dakika 90 za mchezo wa leo zinapaswa kutoa matokeo chanya kwa upande wa Yanga
Ni wazi utakuwa mchezo mgumu kwani hata wenyeji Namungo Fc wamepoteza mechi mbili zlizopita, leo wanacheza katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Yanga ambayo wanaamini wanaimudu
Mashabiki wa Namungo Fc wamesikika wakitamba akiwemo mlezi wa timu hiyo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ambay pia ni Mbunge wa jimbo la Ruangwa
Lakini Yanga kufungwa leo itamaanisha Wananchi watakubali kupoteza mechi ya nne mfululizo
Ahadi waliyotoa wachezaji wa Yanga kwa mashabiki wao ni kuwa leo wanarudisha tabasamu katika nyuso zao