Ukiangalia takwimu za MC Alger za mechi sita zilizopita katika masindano yote, wameshinda mechi moja, kutoka suluhu mechi nne na kupoteza mechi moja
Katika mechi hizo sita, MC Alger wamepachika mabao mawili tu wakishindwa kufunga bao lolote katika mechi mbili za mwisho ambazo zote walilazimishwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Nao wamepita katika kipindi kigumu cha kupata matokeo katika mechi za karibuni pengine ndio sababu walitaka kuhamisha mchezo dhidi ya Yanga kutoka dimba la Julai 05 1962 kupeleka Douera
Hii ni mechi ambayo kama kocha Sead Ramovic atachanga karata zake vyema, Yanga inaweza kuchukua alama tatu ugenini na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania tiketi ya kutinga robo fainali
Baada ya ushindi wa mabao 2-0 ambao Yanga waliupaata dhidi ya Namungo Fc, ari na morali ya wachezaji iko juu na sasa jukumu lao ni kuhakikisha wanarudisha alama tatu walizopoteza katika mechi ya kwanza dhidi ya Al Hilal
Yanga inatarajiwa kuwasili Algiers leo ambapo watakuwa na takribani siku tatu za kukamilisha maandalizi kabla ya mchezo huo utakaopigwa Jumamosi saa nne usiku