Leo majira ya saa 4 usiku saa za Tanzania, mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga watakuwa uwanjani pale July 05 1962 kumenyana na MC Alger katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Hii ni mechi muhimu sana kwa Yanga kuhakikisha ushindi au hata matokeo ya sare yanapatikana ugenini kuweka hai malengo ya kusonga mbele katika hatua inayofuata katika michuano hiyo
Yanga imekuwa na wakati mzuri wa maandalizi huko Algeria jana ikifanya mazoezi yake ya mwisho dimba la July 05 ambapo mchezo huo utapigwa
July 05 sio uwanja mgeni kwa Yanga kwani ni katika uwanja huo mchezo wa fainali kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ulipigwa Juni 02 mwaka jana
Kitu cha tofauti katika mchezo wa leo ni kutokuwepo kwa mashabiki kwani klabu ya MC Alger inatumikia adhabu ya kutoingiza mashabiki katika mechi mbili uwanja wa nyumbani kutokana na vurugu walizofanya kwenye mchezo wa kuwania kutinga makundi dhidi ya US Monastir
Kila la kheri Wananchi...!