Kazini kwa Ramovic kuna kazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Dec 2024
Kazini kwa Ramovic kuna kazi

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic kwa sasa anazongwa na kulaumiwa kufuatia mwenendo mbaya wa kikosi chake katika michuano ya ligi ya mabingwa

Jana Ramovic alipoteza mechi yake ya pili mfululizo katika michuano hiyo baada ya Yanga kufungwa mabao 2-0 na MC Alger

Ni matokeo ambayo yamewakatisha tamaa Wananchi lakini kocha huyo raia wa Ujerumani anaamini timu yake bado ina nafasi ya kurejea katika ubora na kufanya vizuri katika mechi zitakazofuata

Ramovic anakabiliwa na kazi ngumu ya kubadili upepo ndani ya muda mfupi, anachohitaji ni uungwaji mkono tu kwani hakuna muujiza ambao utaitoa Yanga hapa ilipo zaidi ya kazi kufanyika katika uwanja wa mazoezi

Ramovic alikabidhiwa Yanga ikiwa 'imechoka' bahati mbaya kwake hakupata muda wa kutosha kukiandaa kikosi baada ya Miguel Gamondi kufutwa kazi

Mbaya zaidi kikosi chake kimecheza mechi za Kimataifa kikiwakosa baadhi ya wachezaji muhimu

Khalid Aucho, Clement Mzize, Chadrack Boka na Dickson Job jana hawakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya MC Alger kutokana na changamoto zinazowakabili

Aucho, Boka na Mzize wamekosa mechi zote tatu ambazo Ramovic ameiongoza Yanga mpaka sasa

Pengine ataweza kuwatumia nyota hao katika mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe baada ya afya zao kuimarika

Ramovic pia ana kazi ya kuimarisha viwango vya baadhi ya wachezaji ambao msimu huu hawaonekani kuwa katika ubora

Stephane Aziz Ki alikuwa injini ya mabao ya Yanga msimu uliopita lakini iko wazi msimu huu hajaonyesha hata robo ya kile alichofanya msimu uliopita

Prince Dube nae hajafikia matarajio ya wengi katika eneo la ushambuliaji huku Jean Baleke akishindwa kuonyesha ushawishi katika kiwanja cha mazoezi

Ni kama Ramovic amemuondoa Baleke katika mipango yake na huenda nyota huyo akarejeshwa katika klabu yake ya TP Mazembe pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’