Chama anaitaka namba kikosi cha kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Dec 2024
Chama anaitaka namba kikosi cha kwanza

Katika mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger, kiungo mshambuliaji Clatous Chama aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Stephane Aziz Ki ambaye ni sahihi kusema bado 'gari halijawaka' msimu huu

Kuingia kwa Chama na baadae Prince Dube kulileta mabadiliko katika eneo la ushambuliaji ambapo katika dakika 10 za mwisho Yanga ilicheza vizuri zaidi na pengine Chama angeweza kufunga moja ya nafasi adimu na hata kusababisha mkwaju wa penati katika majaribio yake kadhaa kama waamuzi wangekuwa makini

Chama pia alibadili kasi ya mchezo alipoingia mechi ya ligi kuu dhidi ya Namungo Fc na alitoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Pacome Zouzoua

Chama ni kama amemtumia ujumbe kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic kuwa anastahili kuanza katika kikosi chake

Kwa sasa Chama anaonekana kuwa katika kiwango bora pengine kuliko hata Aziz Ki ambaye ana kazi ya kufanya kurejea katika ubora alioonyesha msimu uliopita

Lakini pia Chama ameonyesha kuwa na maelewewano mazuri ya kiuchezaji anapocheza na Pacome Zouzoua

Ukiacha mechi dhidi ya Namungo, mechi nyingine ambao wawili hao walishirikiana vyema ilikuwa dhidi ya Pamba Jiji mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0

Katika mchezo huo Chama alitengeneza bao lililofungwa na Pacome huku pia mwenyewe akifunga bao kupitia mpira wa faulo

Mabao matatu aliyofunga Pacome kwenye ligi msimu huu, mawili yamepita katika mguu wa Mwamba wa Lusaka

Kwa kiwango alichoonyesha Chama katika mechi za karibuni, haitashangaza kama Ramovic atamuanzisha katika mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Lubumbashi Jumamosi ya wiki hii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’