Mechi nne za kuirejesha Yanga kileleni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Dec 2024
Mechi nne za kuirejesha Yanga kileleni

Baada ya kukamilisha mechi ya raundi ya tatu ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe na kupata alama moja muhimu ugenini, matokeo ya sare ya bao 1-1, Yanga imeiweka TP Mazembe kiporo na sasa inaelekeza nguvu zake katika mechi nne za ligi kuu zitakazopigwa ndani ya siku 10

Alhamisi Disemba 19 Yanga itashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili Mashujaa Fc. Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga katika uwanja wake mpya wa nyumbani, KMC Complex

Siku tatu baadae, Disemba 22 Yanga itarudi tena KMC Complex kumenyana na Tanzania Prisons kabla ya kusafiri mkoani Dodoma kuikabili Dodoma Jiji Disemba 25 katika uwanja wa Jamhuri

Disemba 29 Yanga itarejea tena KMC Complex kuhitimisha mwaka 2024 kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanahitaji kuvuna alama 12 katika mechi hizo lengo likiwa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi

Kamwe ameongeza kuwa mechi hizo pia watazitumia kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa raundi ya nne hatua ya makundi CAF CL dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Januari 03 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’