Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema mechi ya ugenini ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe imempa mwanga kuona ni kwa kiasi gani wachezaji wake wameanza kuelewa kile ambacho wanapaswa kufanya
Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Yanga iililazimika kusubiri hadi dakika za majeruhi kusawazisha kupitia bao la Prince Dube
Vijana wa Ramovic walionekana kuwa bora zaidi katika kipindi cha pili wakitengeneza nafasi nyingi kuliko wenyeji wao
Ramovic amesema mechi yake bora tangu alipotua Yanga ni mechi hiyo dhidi ya TP Mazembe
"Ilikuwa mechi nzuri, tulifanya mambo mengi kwa usahihi, nafikiri tangu nimefika Yanga nadhani hii ndio mechi bora kuwahi kucheza dhidi ya TP Mazembe"
"Tulimsoma vyema mpinzani wetu tukajua ubora na mapungufu yake. Nadhani tulipaswa kufunga mabao matatu au manne kwa nafasi tulizotengeneza," alisema Ramovic muda mfupi baada ya kutua kutoka DR Congo
Ilikuwa mechi ya nne kwa Ramovic kukiongoza kikosi cha Yanga, akipoteza mechi mbili, kushinda moja na sare moja
Ramovic atakuwa na mechi nyingine nne zinazofuata kwenye ligi kabla ya mchezo wa marudiano dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Januari 03 2025