Matchday: Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Dec 19

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2024
Matchday: Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Dec 19

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wako uwanja wa KMC Complex kuikabili Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Itakuwa mechi ya kwanza kwa Yanga kucheza katika dimba la KMC Complex wakiwa wamehama kutoka Azam Complex

Lakini pia itakuwa mechi ya pili ya ligi kwa kocha Saed Ramovic ambaye mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Namungo Fc mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 2-0

Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo katika uwanja wa nyumbani, Yanga hawapaswi kudondosha alama zaidi nyumbani ili kuhakikisha wanabaki katika malengo ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi kwani Mashuja Fc ni miongoni mwa timu ngumu msimu huu ikipata matokeo mazuri inapocheza nyumbani au ugenini

Baada ya Yanga kuyumba katika mechi chache zilizopita, mwenendo huo ni kama umeondoa woga kwa timu pinzani na haishangazi kuona hata Mashujaa Fc kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii tambo zimetawala kuelekea mchezo huo

Wachezaji wa Yanga leo wanapaswa kuhakikisha alama tatu zinamilikiwa na Wananchi lakini pia kuonyesha kandanda safi ambalo litarejesha heshima ya Yanga mitaani na kuwaziba midomo 'wachambuzi wa mchongo' ambao kula yao ni Yanga inapofanya vibaya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’