Yanga imeendeleza ubabe ligi kuu ya NBC leo ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi na ilihitaji dakika 12 kufunga bao la uongozi kupitia kwa Clement Mzize aliyemalizia pasi murua kutoka kwa Prince Dube
Wananchi waliendelea kutawala mchezo huo na kuongeza mabao mengine mawili kabla ya mapumziko kupitia kwa Prince Dube na Ibrahim Bacca
Kipindi cha pili Yanga ilipunguza kasi ikicheza kwa tahadhari kubwa huku Tanzania Prisons wakitumia mipira mirefu kushambulia baada ya kushinda kuipenya ngome ya Yanga
Bacca akaiongezea Yanga bao la nne dakika za lala salama akimalizia krosi ya Pacome Zouzoua hilo likiwa bao lake la nne msimu huu
Bacca na Dube sasa ndio vinara wa mabao katika kikosi cha Yanga wakiwa wamefunga mabao manne
Bacca leo amebeba tuzo ya mchezaji bora wa mechi baada ya kufunga mabao mawili
Ushindi huo unairejesha Yanga nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikifikisha alama 33 ikiwa juu ya Azam Fc kwa tofauti ya mabao