Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wako mkoani Dodoma kuikabili Dodoma jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Mechi nyingine muhimu kwa kikosi cha kocha Sead Ramovic kuendelea kukusanya alama tatu ili kusogea karibu ya mtani wake Simba
Wakazi wa Dodoma leo wamepata bahati kubwa ya kushuhudia 'Gusa, achia twende kwao' katika siku hii ya Christimas
Yanga ilitua Dodoma juzi, jana kikosi kikakamilisha maandalizi yake katika dimba la Jamhuri
Haitakuwa mechi nyepesi lakini ili kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo, Yanga inapaswa kushinda mechi ngumu
Upinzani ni mkali msimu huu, hakuna tena nafasi ya kudondosha alama 'kizembe' kama livyotokea katika mechi mbili ambazo Yanga walipoteza
Kila la kheri Wananchi....!
ADVERTISE HERE