Yanga imeendelea kugawa dozi ligi kuu ya NBC leo ikiichapa Dodoma Jiji mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wwa Jamhuri mkoani Dodoma
Ilikuwa siku ya shoo za Clement Mzize huku Prince Dube akiendeleza kasi ya kuzifumania nyavu
Mzize alifunga bao la uongozi dakika ya 19 akimalizia kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Aziz Ki
Aziz Ki akaongeza la pili dakika ya 29 kupitia mkwaju wa penati baada ya Dube kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari
Yanga iliendelea kulisakama lango la Dodoma Jiji, Mzize akiongeza la tatu baada ya makosa yaliyofanywa safu ya ulinzi ya Dodoma Jiji
Msumari wa nne uliwekwa kambani na Dube dakika ya 63 akimalizia pasi ya Mudathir Yahya
Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe alama 36, alama moja nyuma ya watani zao Simba
ADVERTISE HERE