Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra ni miongozi mwa wachezaji wanaojifua yakiwa ni maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Jumamosi, Januari 04
Baada ya kukosekana katika kikosi cha Yanga kwa takribani wiki tatu, Diarra amerejea katika wakati sahihi kuelekea mechi hiyo dhidi ya TP Mazembe
Nyota huyo raia wa Mali alikuwa akisumbuliwa na tatizo la misuli akiumia katika mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya Mazembe
Kurejea kwake ni habari njema kwa Yanga, uzoefu wake katika michuano ya Kimataifa ni silaha muhimu kwa Yanga kuelekea mchezo huo ambao Wananchi wanahitaji ushindi

ADVERTISE HERE