Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize
Ni sahihi kusema kwa sasa ni mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Yanga kutokana na kazi yake nzuri anayofanya
Tangu ujio wa kocha Sead Ramovic, Mzize yuko 'onfire'akipachika mabao sita kwenye mashindano yote huku akitoa assist mbili
Kama TP Mazembe hawatafuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, kwa hakika hawatalisahau jina la Mzize kwani ndiye atakayekuwa amefuta matarajio yao akipachika mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 ambao Yanga walipata mwishoni mwa wiki
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
ADVERTISE HERE