Tutawaheshimu Al Hilal - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2025
Tutawaheshimu Al Hilal - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema hatma yao ya kufuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika imeshikiliwa na mechi mbili zilizobaki wakianza na mchezo dhidi ya Al Hilal

Kamwe amesema kuwa inabidi waende Mauritania kwa tahadhari na kucheza mechi kwa mahesabu makubwa kutokana na ugumu na umuhimu wa mchezo huo ambao kwao hauhitaji chochote zaidi ya ushindi

"Tunakwenda huko kwa ajili ya kusaka pointi tatu tu na si vinginevyo, tutakwenda kucheza kwa tahadhari kubwa kulingana na ubora wa mpinzani wetu"

"Hatutakwenda kufunguka sana kwa sababu Al Hilal ni timu yenye ubora zaidi linapokuja suala la mashambulizi ya kushtukiza, ni mechi ngumu ambayo inabidi twende kucheza kwa mahesabu makali kwani hatuna tunachohitaji zaidi ya ushindi"

"Tukipata pointi tatu basi tutakuwa na matumaini kwa sababu mechi yetu ya mwisho dhidi ya MC Alger tutacheza tukiwa nyumbani," alisema Kamwe

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini Alfajiri ya kesho Alhamisi kuelekea Mauritania tayari kwa mchezo huo huku Wananchi wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Al Hilal wana historia ya kuisumbua Yanga kila timu hizo zilipokutana ambapo Yanga haijapata ushindi dhidi yao katika mechi tatu za mwisho

Yanga inahitaji kushinda mechi inayofuata ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’