Yanga yashauriwa kucheza kwa tahadhari Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
3 May 2018
Yanga yashauriwa kucheza kwa tahadhari Algeria
Kikosi cha Yanga kinaondoka leo kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USm Alger.

Mchezo huo wa kundi D utapigwa Jumapili ijayo, May 06.

Yanga inakwenda Algeria ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa mwisho iliyocheza nchini humo mwaka jana kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya MC Alger.

Ukiachilia mbali 'figisu' za hapa na pale, timu za waarabu zimekuwa zikijipanga kikamilifu kuhakikisha zinapata ushindi katika ardhi yao.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe amesema mbali na mbinu za nje ya uwanja, timu za kiarabu zina kiwango bora.

“Yanga ijipange ihakikishe timu yao iko fiti hata kucheza dakika 120 kocha ana wajibu wa kuangalia mfumo mzuri wa kuwapa matokeo, nadhani mashambulizi ya kushitukiza yatafaa,” Mwakingwe ameliambia gazeti la Mwanaspoti.

Kocha wa makipa wa Yanga na kipa wa zamani wa Taifa Stars, Juma Pondamali alisema tofauti iliyopo na timu za kiarabu ni maandalizi.

“Kuna timu wachezaji wanaambiwa mkishinda mnapewa Dola 10,000, mkichukua kombe mnaongezewa Dola 10,000 unadhani kitakachotokea ni nini kama sio timu kupambana kufa na kupona, ndivyo wanavyofanya wenzetu,” alisema Pondamali.

Nyota wa zamani wa Taifa Stars, Adolph Rishard alisema mbinu itakayoivusha Yanga ni kucheza soka la kumiliki mpira.

“Sio mbinu ya kupaki basi, wajaribu kuiga Barcelona au Real Madrid soka lao wanalocheza, pia wawe na nidhamu ya hali ya juu katika mchezo,” alisema Rishard.

Alisema Waarabu wako mbali kwenye mbinu na ufundi wa mpira lakini akasisitiza kama Yanga ikijipanga na kuwa na nidhamu ya hali ya juu ya mchezo watafanya vizuri.

“Enzi zetu tuliwafunga Waarabu, sijui kizazi cha sasa kina nini, ila ninachokiona jamaa wanatushika kwenye nidhamu ya mchezo,” alisema Rishard.

Naye kipa wa zamani wa Simba, Mohammed Mwameja ameitaka Yanga kupambana kucheza kufa au kupona kupata hata matokeo ya sare kama itakosa ushindi, lakini isikubali kufungwa idadi kubwa ya mabao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1m ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE →