TP Mazembe yatupwa nje CAF CL kundi A

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2025
TP Mazembe yatupwa nje CAF CL kundi A

TP Mazembe imekuwa timu ya kwanza kutupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa kundi A baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa MC Alger hapo jana

Mazembe walihitaji kushinda mchezo huo uliopigwa Algeria jana lakini bao la mkwaju wa penati kipindi cha kwanza liliwapa MC Alger alama tatu nyumbani na kuwakatia Mazembe tiketi ya kurudi nyumbani

Matokeo hayo pia yanamaanisha Yanga haipaswi kupoteza mchezo dhidi ya Al Hilal hapo kesho ili kuweka hai matumaini ya kufuzu robo fainali

Al Hilal inayoongoza kundi A ikiwa alama 10, tayari imefuzu huku MC Alger wakiendelea kushikilia nafasi ya pili wakiwa na alama 8

Yanga ni ya tatu ikiwa na alama 4 wakati TP Mazembe wanaburuza mkia wakiwa na alama 2

Kama Yanga itapoteza mchezo dhidi ya Al Hilal hapo kesho, itaungana na TP Mazembe kuondoshwa katika michuano hiyo kwani hata ikishinda mechi ya mwisho dhidi ya MC Alger itafikisha alama 7 ambapo tayari MC Alger wana alama 8

Yanga inahitaji kushinda mechi mbili zilizobaki ili kufuzu robo fainali moja kwa moja na kama ikitoka sare dhidi ya Al Hilal, itahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0 dhidi ya MC Alger ili kufuzu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’