Jana Stephane Aziz Ki alifunga bao muhimu la ushindi dhidi ya Al Hilal na kuiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa
Yanga inahitaji kushinda mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi dhidi ya MC Alger utakaopigwa Jumamosi, Januari 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Lilikuwa bao lake la pili katika kampeni ya ligi ya mabingwa kuanzia hatua ya makundi msimu huu, akiwa sawa na Clement Mzize aliyefunga mabao yake katika mchezo dhidi ya TP Mazembe
Katika mchezo wa jana, Yanga ilipiga mashuti matano yaliyolenga lango, manne yalipigwa na Aziz Ki
Kwa sasa unaweza kusema MVP huyo wa ligi kuu ya NBC msimu uliopita amerejea katika ubora wake baada ya kuanza msimu taratibu
ADVERTISE HERE