Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wanatupa karata muhimu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL) pale watakapoumana na MC Alger katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi
Dakika 90 za mchezo huo zinabeba hatma na matarajio ya Yanga kucheza robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo
Ni ushindi pekee ambao utaipa Yanga nafasi ya kufuzu robo fainali huku wapinzani wao wakihitaji sare tu
Unaweza kusema leo pale dimba la Mkapa yanahitajika matokeo ya aina moja tu, Yanga ishinde au MC Alger wapoteze na si vinginevyo
Hii ni mechi ya kuiheshimisha Yanga katika mashindano ya CAF msimu huu kwani kama watafanikiwa kutinga robo fainali, watapanda hadi nafasi ya tano katika 'ranking' za CAF na kuwapiku watani zao Simba ambao kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakitambia nafasi yao CAF
Kwa wachezaji hii ni mechi yenye thamani kubwa kwani ushindi utawahakikishia kuvuna kiasi kikubwa che fedha. Endapo Yanga itatinga robo fainali, itakuwa na uhakika wa kuvuna zaidi ya Tsh bilioni 2.3
Mechi hii pia inahitaji nguvu kubwa ya mashabiki, muitikio wa Wananchi kununua tiketi ni mkubwa, bila shaka dimba la Mkapa leo litakuwa 'full house'
MC Alger watakutana na 'taswira ya kutisha' pale uwanja wa Benjamin Mkapa, mechi hii imesubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Yanga
Ni dakika 90 za kivumbi na jasho, Yanga itagusa, itaachia na itaenda robo...!
Kila la kheri Wananchi....!