Mashabiki wa Yanga wameendelea kumiminika uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger ambao utapigwa saa 10 jioni
Wananchi wanasema leo kazi ni moja tu dimba la Mkapa, kukamilisha hesabu za kutinga robo fainali
Yanga inashika nafasi ya tatu kundi A ikiwa na alama 7, ushindi utawafanya Wananchi wafikishe alama 10 na kukata tiketi ya robo fainali
Hii ni mechi ya kulinda heshima ya Yanga na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano ya CAF
GUSA ACHIA TWENDE ROBO FAINALIIII....!




ADVERTISE HERE