Kiungo mshambuliaji wa Yanga Jonathan Ikangalombo ameisubiri kwa hamu mechi yake ya kwanza kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara
Ikangalombo alitua Yanga katika dirisha dogo lililofungwa Januari 15, pengine kesho Jumamosi kocha Sead Ramovic anaweza kumtumia kwa mara ya kwanza katika mchezo wa raundi ya pili kombe la CRDB dhidi ya Copco Fc utakaopigwa dimba la KMC Complex
Winga huyo ambaye pia anamudu kucheza kama straika, amesema anatamani kuanza kuitumikia timu hiyo ili atoe mchango wake pia akieleza kuumizwa na matokeo ya mechi dhidi ya MC Alger ambayo yalisababisha Yanga isifuzu robo fainali ligi ya mabingwa
Nyota huyo aliyetua Yanga akitokea klabu ya AS Vita ya DR Congo,Β hakutumika katika mechi dhidi ya MC Alger kwa vile alishaitumikia AS Vita katika mechi za awali za Kombe la Shirikisho Afrika na kibarua chake kipo katika mechi za mashindano ya ndani
"Nilikuwa naumia wakati nikiwa jukwaani kwani, niliona nina kitu ambacho kingeisaidia timu yangu, lakini kwa vile kanuni zilikuwa zinanizuia, sasa naomba nipewe mechi hizi za michuano ya ndani tuitafute tiketi ya CAF kwa msimu ujao," Ikangalombo alinukuliwa na Mwanaspoti