Tukio kubwa la kihistoria lilifanyika nchini Morocco jana ambapo Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la vilabu Barani Afrika (ACA), alikabidhiwa jengo la ofisi ya ACA na Rais wa Soka la Morocco, Fouzi Lekjaa
Baada ya makabidhiano hayo na utiaji saini wa makubaliano ya pande zote mbili, hafla rasmi ya uzinduzi wa ofisi hizi itafanyika leo Jumanne Januari 28, 2025
Hersi amesema baada ya hatua hiyo, ni wakati wa kuanza kufanya kazi ya vilabu na kujenga uimara kwa maslahi mapana ya mpira wa miguu
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Hersi ameandika ujumbe huu;
"Leo ni siku ya kihistoria katika maendeleo ya mpira na vilabu barani Afrika kwa kusaini makubaliano ya kuweka MAKAO MAKUU YA UMOJA WA VILABU BARANI AFRIKA.
Makao haya makuu yatakuwa hapa RABAT katika complex ya MOHAMMED VI huku yakipakana na ofisi za CAF na FIFA.
Sasa ni wakati wa kuanza kufanya kazi ya vilabu na kujenga uimara kwa maslah mapana ya mchezo huu pendwa duniani.
Shukran za dhati jwa wenyeji wetu, shirikisho la mpira la Falme ya Morocco, hususan Rais FOUZI LEKJAA"



