Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli
Unapozungumzia wachezaji ambao wamejitengenezea heshima kubwa mbele ya mashabiki wa Yanga, Maxi ni mmoja wa wachezaji hao
Akiwa katika msimu wake wa pili na Wananchi, Maxi hana deni kwani ni mchezaji anayejitoa kwa moyo wote kila anaposhuka uwanjani kuitumikia Yanga
Alianza vyema msimu huu lakini akapata majeraha ambayo yalimuweka nje kwa takribani mwezi mzima na kumfanya akose mechi tatu muhimu za Yanga katika ligi ya mabingwa
Sasa amerejea kuendelea kuipambania nembo ya Yanga ambapo yeye na wachezaji wengine wanapaswa kuhakikisha Yanga inatetea taji la Ligi Kuu na kombe la Shirikisho la CRDB
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
Happy Birthday Maxi...!