Haiwezekani timu moja iwe na matukio ya utata kila mechi - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Feb 2025
Haiwezekani timu moja iwe na matukio ya utata kila mechi - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amezitaka mamlaka za usimamizi wa soka nchini kufanyia kazi malalamiko na maoni ya wadau kuhusu kukithiri kwa matukio ya makosa ya kibinadamu ya marefa hasa katika mechi zinazohusisha klabu ya Simba

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;

"Leo Asilimia 90 ya mijadala iliyofanywa kwenye vipindi vya Michezo, Wachambuzi wamejadili kuhusu Makosa ya Waamuzi kwenye mechi ya Kolo.

Na leo sio mara ya kwanza, Huu ni muendelezo. Ni kama Mechi ya 10 Mfululizo, Kila mechi ya Kolo huwa na Mijadala redioni kuhusu Makosa ya Waamuzi yanayowanufaisha KOLO kupata Ushindi

Mara wapinzani wanayimwa Magoli Halali, Mara mjadala wa Kolo akifunga Magoli ya Offside na waamuzi wanayakubali. Tumesikia pia Mijadala ya Penalti nyingi za mchongo zikiwanufaisha Makolo.

This is Is Too Much .. Na inatupa Wasiwasi kama Haya Yanayotokea, huwa yanatokea kwa Bahati mbaya kwa kichaka cha ‘Makosa ya Kibinadamu’

Tafadhali, Wenye Mamlaka naamini mnaona na kusikia yanayojadiliwa kuhusu Mpira wetu.

Hii mijadala inayoendelea sasa kwenye Media, Sio tu kwamba inapunguza ladha ya mpira wetu, Bali inatia Doa nguvu kubwa mnayoifanya kuhakikisha Mpira wetu unapanda na unakuwa na mvuto Afrika.

Tafadhali sana .. Tunahitaji kusikia sauti zenu wenye Mamlaka juu ya hiki kinachoendelea kwa sasa.

Haiwezekani Timu moja tu iwe na Matukio ya Utata kwenye Mechi zaidi ya 10"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’