Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili KenGold katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC
Yanga leo itashuka KMC Complex kucheza mechi hiyo ikiwa na benchi jipya la ufundi baada ya Sead Ramovic aliyekuwa Kocha Mkuu kuondoka pamoja na Kocha Msaidizi Mustafa Kodro
Hata hivyo tayari Yanga imemuajiri Kocha Miloud Hamdi aliyeinoa Singida Black Stars kwa siku 36 ambapo atasaidiana na AbdulHamid Moallin ambaye licha ya majukumu yake ya Ukurugenzi wa ufundi, Yanga ilimuongezea majukumu mengine ya kusaidia katika benchi la ufundi
Ni wazi mabadiliko hayo ya benchi la ufundi yaliyofanywa jana hayawezi kuwa na athari kwa Yanga kuelekea mchezo dhidi ya KenGold kwani Ramovic alikamilisha maandalizi yote ya mchezo huo kabla ya kuaga jioni ya jana
Ni mechi ambayo Yanga inahitaji kushinda ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi
KenGold ni timu mpya ikisajili takribani wachezaji 24 kwenye dirisha dogo, hii itakuwa mechi yao ya kwanza ya mashindano
Timu hiyo inawajumuisha nyota waliowahi kuitumikia Yanga akiwemo nahodha wao Kelvin Yondani
Wengine ni Zawadi Mauya, Obrey Chirwa, Erick Kabamba na Bernard Morrison ambaye hata hivyo atakosa mchezo huo akiwa majeruhi