Mshambuliaji hatari wa Yanga Amissi Tambwe amesema mazoezi makali wanayoyapata sasa kutoka kwa kocha George Lwandamina yatamuwezesha kuwa moto wa kuotea mbali ligi ikianza na amejipanga kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.
Tambwe ameyazungumza hayo leo asubuhi kwenye mazoezi ya kikosi cha Yanga mkoani Morogoro.
Tambwe amesema wameifurahia kambi yao mkoani Morogoro na mazoezi wanayofanya yatawawezesha kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya Kimataifa baadae.
Kikosi cha Yanga kiko mkoani Morogoro kwenye kambi maalumu ya kuwajenga wachezaji tayari kwa mikikimikiki ya ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Muhimu zaidi, Agosti 23 kutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Simba.

ADVERTISE HERE