Kiungo mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib leo amekuwa baba baada ya mkewe kujifungua mtoto wa kike.
Ajib ameelezea furaha yake baada ya mkewe kujifungua salama. Amesema alikuwa na hofu juu ya hali yake kabla ya Mwenye ez Mungu kumjaalia kujifungua.
Katika hatua nyingine, Ajib ameeleza masikitiko yake kwa baadhi ya mashabiki wanaomshambulia kuwa amegoma kusafiri na kikosi cha Yanga nchini Algeria.
Amesema kwa hali aliyokuwa nayo mkewe kabla ya kujifungua asingeweza kutimiza majukumu yake ipasavyo kutokana na matatizo ya uzazi yaliyokuwa yakimsumbua mkewe.
Amesema mpira ni kazi yake na hawezi kugoma kutimiza wajibu wake kama mchezaji.

ADVERTISE HERE