Yanga imeendeleza vipigo dimba la KMC Complex leo ikiibamiza KMC mabao 6-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi Yanga ikitawala, KMC wamshukuru mlinda lango kwani leo wangekumbana na kipigo cha aibu
'Bwana Harusi' Stephane Aziz Ki amekuwa mchezaji wa pili kufunga hat-trik msimu huu akiweka kambani mabao matatu, mawili yakiwa mikwaju ya penati
Aziz Ki amefanyia kazi mapungufu yake katika upigaji wa 'matuta' na leo akaweka kamba mbili za penati
Prince Dube akiwa katika kiwango bora, leo amefunga bao lake la nane na kutoa assist 3 na hivyo kuhusika katika mabao manne
Maxi Nzengeli na Israel Mwenda wakafunga mabao mengine dakika za lala salama kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu zinazowarudisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Ni ushindi wa pili wa mabao 6 Yanga inaandikisha katika dimba la KMC Complex