Kwa sasa ukizungumzia washambuliaji bora katika ligi kuu ya NBC utawataja nyota wawili wa Yanga Clement Mzize na Prince Dube
wakati Mzize akiwa katika msimu wake wa tatu na Yanga, Dube ametua kwa Mwananchi msimu huu akitokea klabu ya Azam Fc
Unaweza kusema mwanzo wake kwenye ligi ulikuwa wa kusuasua, wapinzani wake wakatumia mwanya huo kuponda usajili wake na kumshusha thamani
Lakini mpaka sasa tayari Dube amefanya mambo mazuri ndani ya kikosi cha Yanga akiwa na takwimu nzuri
Ubora wake msimu huu akiwa na Yanga, tayari amehusika katika mabao 16 kati ya 50 yaliyofungwa na kikosi hicho kizima kwenye Ligi Kuu Bara ambapo amefunga tisa na kutoa 'asisti' saba huku akipitwa bao moja tu na Mzize mwenye mabao 10 na asisti 4
Pacha yake na Mzize imeanza kuwapa changamoto wapinzani kwani kwa wastani wachezaji hao wanahusika katika mabao kwenye kila mechi
Kama hawakufunga basi watashiriki katika kutengeneza mabao, haishangazi kuona wawili hao wamehusika katika mabao 30 wakifunga mabao 19 na kutoa asisti 11 kwa pamoja