Yanga imeendeleza ubabe wake katika ligi kuu yaa NBC leo ikishusha kipigo kizito kwa Mashujaa Fc kwa ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika
Licha ya kuwa ugenini, Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi na alikuwa Duke Abuya aliyefungua kalamu ya mabao baada ya kunasa mpira ndani ya eneo la hatari
Yanga iliongeza mabao manne katika kipindi cha pili kupitia kwa Prince Dube, Khalid Aucho huku Clatous Chama aliyeingia kipindi cha pili akiweka kambani mabao mawili
Ni ushindi wa thamani kubwa kwa Yanga ugenini kwani alama hizi tatu zimeifanya Yanga izidi kujiimarisha juu ya msimamo baada ya kufikisha alama 55
Mshambuliaji Prince Dube amefikisha mabao 10 akipanda juu katika mbio za ufungaji boraakiungana na Clement Mzize
Pacome Zouzoua aliyeibuka nyota wa mchezo alitengeneza mabao mawili sasa akifikisha assist 6