Yanga imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba
Pamba Jiji walianza mchezo huo kwa kasi wakilishambulia lango la Yanga lakini ni Wananchi waliotangulia kufunga bao dakika ya 28 kupitia kwa Chadrack Boka aliyefunga mpira wa faulo nje kidogo ya 18
Ilikuwa mechi ambayo kocha Miloud Hamdi aliingia kimbinu zaidi akianza na viungo wa ulinzi watatu Khalid Aucho, Mudathir Yahya na Duke Abuya kukabiliana na presha ya Pamba JijiΒ
Kipindi cha pili Miloud alimuingiza Stephane Aziz Ki nafasi ya Aucho, mabadiliko ambayo yaliifanya Yanga iongeze kasi ya mashambulizi
Ni Aziz Ki aliyekuwa shujaa wa Yanga katika kipindi cha pili akifunga mabao mawili muhimu yaliyoihakikishia Yanga ushindi huo muhimu
Baada ya kusubiri kwa wiki kadhaa, hatimaye leo mashabiki wa Yanga wamemshuhudia winga Jonathan Ikangalombo aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mudathir
Dakika chache alizocheza zilitosha kuonyesha umahiri wake akihusika katika upatikanaji wa bao la pili ambapo alitoa pasi kwa Maxi Nzengeli aliyepiga krosi iliyomaliziwa na Aziz Ki
Ikangalombo alimtengenezea Aziz Ki nafasi nyingine ya wazi ambayo hata hivyo mwamba huyo kutoka Burkina Faso hakuitumia
Alama tatu muhimu kwa Wananchi wakifikisha alama 58 baada ya mechi 22
Kituo kinachofuata ni Kariakoo Derby dhidi ya Simba, March 08