Baada ya kurejea jijini Dar es salaam wakitokea Mwanza, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku moja ambapo kesho Jumatatu wataanza maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni Kariakoo Derby, mchezo ukitarajiwa kupigwa saa 1:15 usiku. Unaweza kusema itakuwa mechi ya maamuzi katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Ushindi kwa Yanga utawahakikishia Wananchi kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Lakini pia utakuwa mwendelezo wa ubabe wa Yanga dhidi ya Simba kwani Wananchi wameshinda mechi zote nne zilizopita dhidi ya Simba
Pengine Derby ya wakati huu itakuwa tofauti na derby nyingine zilizopita kutokana na ushindani uliopo
Tofauti ya alama nne kati ya Yanga na Simba huku Simba wakiwa na mechi moja ya kiporo, zinafanya mchezo huo kuwa mgumu
Itakuwa derby ya kwanza kwa kocha Miloud Hamdi ambaye tangu ajiunge na Yanga kuchukua nafasi ya Sead Ramovic, kikosi chake kimepachika mabao 16 katika mechi 5
Itakuwa mechi ngumu lakini sifa ya timu bingwa ni kushinda mechi ngumu za aina hiyo