Mchezo wa fainali ya Tanzanite Samia Women's Cup 2025 unapigwa leo dimba la Agha Khan ambapo Yanga Princess itamenyana na JKT Queens
Michuano hiyo maalum kuadhimisha siku ya Wanawake ambayo kilele chake ni Jumamosi March 08, imezikutanisha timu nne
Yanga Princess ilitinga fainali kwa kuichapa Fountain Gate Princess mabao 7-0 huku JKT Queens wakitinga fainali kwa kuifunga Simba Queens bao 1-0
Mapema saa 8 uapigwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Simba Queens dhidi ya Fountain Gate Princess na kufuatiwa na mchezo wa fainali saa 10 jioni
Mechi hii ina umuhimu wa kipekee kwa Yanga Princess kwani ushindi utawahakikishia angalau kumaliza msimu huu na kombe

ADVERTISE HERE