Uongozi wa Yanga umetakiwa kushikia msimamo wake kufuatia kitendo cha bodi ya ligi kuahirisha mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mwanasheria, Wakili msomi Simon Patrick amesema uamuzi wa kuahirisha mchezo huo uliochukuliwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ni batili kwa sababu kamati hiyo haina mamlaka ya kujadili mechi ambayo haijachezwa
Simon amesema kilichofanyika ni mkakati wa kuinyima Yanga alama tatu kwa mujibu wa kanuni na kuinusuru Simba kupokwa alama 15 kama kanuni zinavyotaka
Simon amesema viongozi wa Yanga hawapaswi kukubali kucheza mechi hiyo katika wakati mwingine
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema haoni nafasi ya Yanga kucheza mechi nyingine ya ligi msimu huu dhidi ya Simba
Arafat amesema wanachofahamu mechi dhidi ya Simba inapaswa kuchezwa leo kama ilivyopangwa
"Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa kwa msimu wa 2024/25 Yanga itacheza mchezo mwengine wa Derby zaidi ya uliokua umepangwa tar 8/03/2025," alisema ArafatΒ